DARASA LA ELIMU YA MAADILI (DLM)

(Value Education Class-VEC)

Program za Maadili ndani na nje ya Tanzania

vijana wakionyesha kwahusu masomo ya Maadili

Katika programu ya scripture union Tanzania,VOICE Africa Darasa la Elimu ya Maadili (DLM).Tunafurahi kwamba Watu wameipokea programu hii na wanaendelea kupokea Maarifa zaidi ili kufikia watoto,vijana na familia.Darasa hili lina malengo ya Kusaidia kanisa na serikali kuandaa wananchi wenye wajibu na kuchangia mabadiriko ya Maadili ya vijana ,watoto na taifa zima.Itasaidia waalimu kuwa na mtaala mzuri wa ufundishaji ulio rahisi kutumia,wa Kibiblia kwa matumizi yote yafaayo kote kwa madarasa ya shule za Msingi na Sekondari.Kuchochea ufahamu wa kiroho na kimaendelea kwa wanafunzi .Pia itasaidia kuwatia moyo na kuwasaidiawazazi/walezi wa wanafunzi juu ya wajibu wao wa kufundisha maadili kwa watoto.